Hivi ni nini hasa kinaendelea ndani ya TAKUKURU?
December 11, 2007
Hivi ni nini hasa kinaendelea ndani ya TAKUKURU? Hili ndilo swali la kwanza kabisa nililojiuliza baada ya kusoma ujumbe huu. Lakini haijaishia hapo, nikasoma na kutumiwa tena ujumbe huu hapa. Na mambo yote haya yanakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusiana na TAKUKURU.
Madai, tuhuma, minong’ono na mambo mengine kama hayo ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakifukuta chini kwa chini na kusikika mitaani katika siku za karibuni. Bahati mbaya sana ni kuwa hakuna taarifa zozote ambazo zimekuwa zikitoka zenye kueleza hasa nini kinachoendelea.
Waswahili husema kuwa lisemwalo lipo na kama halipo laja. TAKUKURU, ikiwa moja ya Taasisi ambazo Watanzania wamekuwa wakizitolea macho wakiamini kuwa ndio mkombozi wao, haitakiwi kukaa tu kimya bila kusema lolote kuhusiana na masuala hayo yanayosemekana mitaani.
Lakini sio tu kuwa ifungue midomo na kupayuka kukanusha, hapana. Tunataka kupata maelezo ya kina, yenye kueleweka na ambayo yataandaliwa katika mazingira ya kuelewa kuwa Watanzania wamesoma na wanajua kile kinachosemwa kuwa ni uongo au laa.
Nikiwa mmoja wa Watanzania ambao tunaamini kuwa TAKUKURU ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya taifa hili, napenda kusema wazi kuwa TUMECHOSHWA NA HAYA MAMBO NA TUNATAKA MAELEZO YA KUTOSHA KUTOKA TAKUKURU NA SI BLAH BLAH.
Entry Filed under: maskani. .
1 Comment Add your own
Leave a Comment
Some HTML allowed:
<a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <pre> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>
Trackback this post | Subscribe to the comments via RSS Feed

1.
AUGUSTUS FUNGO | December 11, 2007 at 3:25 pm
Habari tunazozisoma kuhushu TAKUKURU na imani tulokuwa nayo juu ya taasisi hii inatuacha hoi kabisa watanzania. Sio habari hii tu ya mpasuko wa ndani ndani ya takukuru yenyewe bali pia hata katika siku ya maadili watanzania walivyoonesha kutokuwa na imani na taasisi hii. Mhe Hosea jisafishe usitafute mchawi,jisafishe wewe na taasisi yako,wekeni mambo hadharani tuwaamini,ili tuache kusikia maneno ya mitaani. Zama za usiri na majungu zimepitwa na wakati watu tunataka kusikia tokakwenye mdomo wa farasi mwenyewe. Mwandishi wa makala hii namsiu sana kwani ameweza kutusemea watanzania nini tunakitaka toka takukuru.Jamani kama mnasoma waraka huu,tupeni majibu.Tumechoka kusikia mahakimu wanakamatwa,wakulima na walimu tunataka sasa mawaziri na makatibu wakuu.Hongera sana msangi