Archive for December, 2007
Happy Maadili Day
Hivi ilikuwa siku ya Maadili au Madili? Anyway, si mbaya lakini, naamini mliifurahia
Add comment December 11, 2007
Hivi ni nini hasa kinaendelea ndani ya TAKUKURU?
Hivi ni nini hasa kinaendelea ndani ya TAKUKURU? Hili ndilo swali la kwanza kabisa nililojiuliza baada ya kusoma ujumbe huu. Lakini haijaishia hapo, nikasoma na kutumiwa tena ujumbe huu hapa. Na mambo yote haya yanakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusiana na TAKUKURU.
Madai, tuhuma, minong’ono na mambo mengine kama hayo ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakifukuta chini kwa chini na kusikika mitaani katika siku za karibuni. Bahati mbaya sana ni kuwa hakuna taarifa zozote ambazo zimekuwa zikitoka zenye kueleza hasa nini kinachoendelea.
Waswahili husema kuwa lisemwalo lipo na kama halipo laja. TAKUKURU, ikiwa moja ya Taasisi ambazo Watanzania wamekuwa wakizitolea macho wakiamini kuwa ndio mkombozi wao, haitakiwi kukaa tu kimya bila kusema lolote kuhusiana na masuala hayo yanayosemekana mitaani.
Lakini sio tu kuwa ifungue midomo na kupayuka kukanusha, hapana. Tunataka kupata maelezo ya kina, yenye kueleweka na ambayo yataandaliwa katika mazingira ya kuelewa kuwa Watanzania wamesoma na wanajua kile kinachosemwa kuwa ni uongo au laa.
Nikiwa mmoja wa Watanzania ambao tunaamini kuwa TAKUKURU ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya taifa hili, napenda kusema wazi kuwa TUMECHOSHWA NA HAYA MAMBO NA TUNATAKA MAELEZO YA KUTOSHA KUTOKA TAKUKURU NA SI BLAH BLAH.
1 comment December 11, 2007

