Archive for November 6th, 2007
Hawa wamepona, wangapi wamekufa?
Ni habari ambayo ilinisikitisha sana kama si kunistua sana kwakweli. Mgonjwa wa kichwa anapasuliwa mguuni na yule wa mguu anapasuliwa kichwani. Sijui nishangae au nijiulize au.
Ikiwa hukukutana na habari hiyo ambayo ilitoka katika gazeti la Mwananchi la siku ya Jumatatu ya Novemba 5, basi bofya hapa uisome habari hiyo kikamilifu na kisha bofya hapa kujua kilichofuatia baada ya habari ile.
Uzembe huu katika Taasisi ya mifupa ya Muhimbili, ni wa aina yake kwakweli, na kwakuwa inaelezwa kuwa yanatokea mambo haya mara kwa mara, tunajiuliza ni wangapi wamepoteza maisha kutokana na uzembe huu?
3 comments November 6, 2007
