Archive for March 18th, 2007

Natafuta funguo

Wapendwa wasomaji, marafiki, wakosoaji na wale wote ambao mmekuwa mkinitembelea kijiweni kwangu kwa muda wote toka nianzishe kijiwe hiki, napenda kuwaomba radhi kwa kuwa kimya kwa muda mrefu kiasi sasa. nakiri kuwa nimekuwa nikikawia sana kuwaletea gumzo jipya mara kwa mara kama ilivyiokuwa awali, lakini mnisamehe sana maana kwakweli nimebanwa na masomo kwa wakati huu. Na kama mnavyojua wahenga walihanikiza “Elimu ni Ufunguo wa Maisha” kwahiyo nimetingwa kidogo na shughuli ya kusaka ufunguo wa maisha yangu.

Nawashukuru sana kwa kuniunga mkono, na nawaahidi kuwa niko pamoja nanyi daima, na pindi masomo yakipungua ukali kidogo, nitajitahidi sana kuwaletea yale mapya niliyokumbana nayo katika safari hii ya sasa.

2 comments March 18, 2007


Bango la Matangazo & Wazo mahususi

Blogi Nyingine

Blogi za Katuni

Blogi za Picha

Malavidavi!

Mapishi

Mavazi & Mitindo

Vyombo vya Habari

wageni

Webu mseto

Blog Stats

 

March 2007
M T W T F S S
« Feb   May »
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  

Archives

Meta

Pages