Ndugu zangu wapendwa!! Nilikuwa na wiki la maojnz…

May 29, 2006

Ndugu zangu wapendwa!!

Nilikuwa na wiki la maojnzi makubwa kwa kumpoteza mmoja kati ya babazangu wakubwa, ambaye alikuwa nguzo muhimu sana kwa familia yetu kwa ujumla. Baba yangu huyo mkubwa, Ally Shaban Msangi, alifariki Jumatatu ya tarehe 22/05/2006, akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akiendelea na matibabu ya tatizo la jino, ambalo lilimsumbua kwa zaidi ya miezi mitatu.

Kwa hali jinsi ilivyo kuwa, kwa hakika pengine hilo ndilo lilikuwa jema kwake yeye, kwa maana alishateseka na maumivu kiasi cha kutosha, lakini kwa namna yoyote ile kifo chake hakika limekuwa pigo kubwa lisilomithilika maishani mwangu na wanafamilia wenzangu kwa ujumla. Ninawashukuru wote wale ambao walishirikiana nami katika kipindi hiki kigumu sana, na hasa rafiki yangu na kipenzi changu Pamella.

Nawashukuru wote kwa ujumla wenu maana ni vigumu sana kuwataja wote hapa, na Mungu atawalipa kwa kila mliloshirikiana nami. Ni njia ya kila mwanadamu kuelekea maisha ya Ahera, na hakika kila mwanadamu ataipita. (Kul-nafsi dhaalikatul mauti)

Tulimpenda sana mzazi wetu, lakini Muumba amempenda zaidi yetu, na tunaamini atamlaza mahali pema peponi mzazi wetu.

Entry Filed under: maskani. .

7 Comments Add your own

  • 1. Boniphace Makene  |  May 31, 2006 at 7:32 am

    Pole Msangi, maisha yake ameyakamilisha na sasa anapumua maana alipokuwa duniani alibena mzigo mzito ambao sasa kautyupa na kuchukua likizo ya mapumziko mema. Nafasi ya mtu hufahamika baada ya kuondoka kwake na kama wataka kutangawa mshindi lazima ukubali kushinda kombe na kulitembeza kila sehemu.

    Pili naomba kufahamu kijana anaitwa Ramadhan Msangi kasoma Mkwawa, Mlimani na sasa yupo Kigoma ni nduguyo maana naye kutoka huko Mbeya?

  • 2. Reginald S. Miruko  |  June 1, 2006 at 9:54 am

    POLE SANA MSANGI. niliandika kwa herufi kubwa nikimaanisha ninachosema na kuwa sina cha kuongezea. lakini hiyo picha imenichanganya.

  • 3. Mija Shija Sayi  |  June 1, 2006 at 11:16 pm

    Pole sana Ramadhani!!

  • 4. SIMON KITURURU  |  June 2, 2006 at 7:15 pm

    Pole Sana Ramadhani!Hata mimi picha ilinichanganya kidogo kuielewa.

  • 5. Jeff Msangi  |  June 5, 2006 at 12:27 am

    Pole sana ndugu yangu,

  • 6. ndesanjo  |  June 7, 2006 at 7:42 pm

    pole sana Rama.

  • 7. Chemi Che-Mponda  |  June 10, 2006 at 5:50 pm

    Pole sana! Kwa kweli, kumpoteza mtu ambaye ni nguzo wa familia ni pigo kubwa sana. POLENI! Mola awape nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.

Leave a Comment

Required

Required, hidden

Some HTML allowed:
<a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <pre> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Bango la Matangazo & Wazo mahususi

Blogi Nyingine

Blogi za Katuni

Blogi za Picha

Malavidavi!

Mapishi

Mavazi & Mitindo

Vyombo vya Habari

wageni

Webu mseto

Blog Stats

 

May 2006
M T W T F S S
« Apr   Jun »
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  

Archives

Meta

Pages